Steve Nyerere amfunda Goodluck Gozbert

DAR ES SALAAM: Msanii wa vichekesho nchini Steve Mengele (Steve Nyerere) amemuandikia ujumbe mzito msanii mwenzake wa muziki wa Injili Goodluck Gozbert baada ya msanii huyo kuchoma moto gari alilopewa kama zawadi na moja ya wahubiri wakubwa wa injili nchini ambaye hata hivyo hakuweka wazi ni nani.
kupitia ukurasa wake wa Instagram, Steve Nyerere ameandika:
“Mstafuuu, Goodluck Gozbert Mdogo wangu kwanza nikwambie Tu mimi ni shabiki yako Miaka nenda Rudi, Una Kipaji Mungu Amekupa tena sio kidogo ni kipaji cha kujivunia sana sana.
Wewe ni Mtaji mkubwa kwenye Nyimbo za Dini Africa Na ulipo kuwa Unaelekea Ulikuwa Diamond Platnumz Katika mziki wa Dini Huo ndio Ukweli,.
Goodluck Gozbert Ulicho kifanya Ni Umeweka Imani Pembeni Umeamini au kumwamini Shetani na kwa hili shetani Ameshinda Tambua Mziki wako ni maubiri Tosha ya kumrudia Mungu,…
Kupitia mziki wako Ulitufundisha kusamehe,
Kupitia mziki wako Ulitufundisha kumwamini Mungu,Kupitia mziki wako Ulitufundisha kufanya Matendo Mema,.
Kupitia mziki wako Ulitufundisha kumkataa Shetani kwa njia yoyote ile,.Kupitia mziki wako Ulitufundisha Kutokuamini Nguvu za Giza kwamba zina Nguvu kuliko Nguvu za Mungu Aliye hai,.
Kupitia mziki Wako Ulitufundisha kupambana na kutokukata Tamaa, Vijana kujitambua na kumuweka Mungu mbele kwa jambo lolote lile.,..
Sikuona sababu ya Kuingia au kufanya Maamuzi ya kuchoma Moto gali bila kutafuta ushauri kwa watu mbali mbali.,.,.
Kwani ilishindikana nini Kuliuza gari na FEDHA hiyo ungetoa sadaka kwa yatima kusali nao kuomba Toba huoni kuwa hata kungekuwa na Mabaya Yangemrudia Mwenyewe.,.
Kuna maskini wangapi wameona Unachoma Moto Gari Ambalo linauzika na ukachukua hiyo FEDHA Ukawapa Yatima, Makundi mbali mbali ya watu wenye Uhitaji,…
Uliwashirikisha wachungaji unayo pitia japo wakuombee na kumshirikisha Mungu Mapito yako,..
Ni kweli Umeamini Maagizo ya shetani nenda kachome Moto gari na ukaenda kufanya hivo,..Hukuwa na muda wa kupambana na shetani,…
Baada ya kuchoma gari una uhakika Utarudi kwenye mfumo wako unaotaka Au kitafata kipi kingine cha kuchoma,…
Rudi kwenye Mazabao Mwambie Mungu Samahani haikuwa Akili yangu ila shetani Alinitangulia waombe msamaha mashabiki wako wanaoamini nyimbo zako ni Injili Tosha,.kwao,..
Wewe ni shujaa bado hujadondoka hivo bali umejikwaa Tu.” ameandika Steve