Mastaa
Mama Imade ajibu tuhuma

LAGOS: Mzazi mwenzake na Staa wa muziki kutoka Nchini Nigeria David Adeleke ‘Davido’, Sophia Momodu amejibu shtaka la Davido la kutaka malezi ya pamoja ya binti yao.
Ikumbukwe kuwa mnamo Juni 2024, iliripotiwa kuwa Davido alifungua kesi akitaka amri ya mahakama impatie ulinzi wa pamoja wa binti yake, Imade, na ufikiaji wake bila vikwazo.
Katika hati ya kukanusha iliyotolewa na wanasheria wa Sophia amekana madai ya Davido kwamba alimnyima kuonana na binti yao.
Alisema kwamba alimnyima tu kupata mwili wake na akakata mawasiliano na binti yao.