Mastaa

Mwanamuziki Liam Payne ajitupa ghorofani na kufa

ARGENTINA: MWANAMUZIKI nyota kutoka kundi la waimbaji wa bendi ya vijana wadogo ya One Direction, Liam Payne amefariki leo asubuhi Oktoba 17 baada ya kujitupa kutoka ghorofa ya tatu, katika hoteli moja jijini Buenos Aires, nchini Argentina.

Payne aliyekuwa anaimba kundi hilo la One Direction amefariki dunia baada ya kuanguka kutoka ghorofa la tatu nchini humo muda mfupi baada ya wafanyakazi wa hoteli hiyo kuita huduma ya dharura kutokana na kuona mabadiliko kwa msanii huyo.

Taarifa za kutisha za simu za dharura ambazo meneja wa hoteli ya Buenos Aires alitoa akiomba usaidizi wa ‘haraka’ kabla ya kifo cha mwimbaji huyo aliyedondoka umbali wa futi 40 asubuhi ya leo.


Mkuu wa mapokezi wa Hoteli ya Casa Sur alipiga simu mbili, akimwambia opereta wa 911 katika simu ya kwanza: “Tuna mgeni ambaye amejitenga kutokana na matumizi ya dawa za kulevya na anaharibu kila kitu chumbani mwake. Tunahitaji mtu aje kwa usaidizi.”

Mazungumzo ya Mkuu huyo yaliendelea kujieleza kwenye simu baada ya kujibiwa “…maisha ya mgeni huyo yako hatarini? Akajibu: “Chumba kina ‘balcony’ na tunaogopa anaweza kufanya kitu.” Sekunde chache baadaye mfanyakazi wa hoteli hiyo, ambaye alijitambulisha kwa jina la kwanza la Esteban, aliongeza: “Tuma tu ambulensi, ambulensi tu.”

Rekodi ya simu ya pili ya huzuni iliyochukua zaidi ya dakika mbili na kuvuja kwa vyombo vya habari usiku kucha, ilianza na opereta wa 911 akisema: “Hujambo, dharura iko wapi?”

Mfanyakazi wa hoteli hiyo alijibu: “Habari za mchana. Nilipiga simu sasa hivi lakini laini ilikufa. Ninapiga simu kutoka kwa Hoteli ya CasaSur Palermo, anwani 6032, Costa Rica.

Mazungumzo yaliendelea huku mashuhuda wa tukio hilo wakidai kwamba simu hazikufanyiwa kazi kwa haraka labda wangeweza kuokoa uhai wa mwanamuziki huyo aliyekuwa akisumbuliwa na ulevi wa dawa za kulevya na pombe.

Related Articles

Back to top button