Kwingineko

Solskjaer kuwaiba hawa Man United

ISTANBUL:OLE Gunnar Solskjaer amerudi rasmi kwenye ukocha baada ya zaidi ya miaka mitatu tangu kuondoka Manchester United. Kocha huyo wa raia wa Norway ameteuliwa kuwa mkufunzi mkuu wa Besiktas, klabu kubwa ya Uturuki.
Besiktas wako nyuma kwa pointi 20 dhidi ya vinara Galatasaray, lakini Solskjaer anaweza kupata msaada kutoka kwa wachezaji wa zamani wa Man United:
Marcus Rashford, mshambuliaji mwenye miaka 27, ameondolewa kabisa kwenye kikosi cha Manchester United na anahusishwa na AC Milan na Borussia Dortmund. Akiwa chini ya Solskjaer, alicheza mechi 135 na kufunga mabao 55 – idadi kubwa zaidi chini ya kocha yeyote katika maisha yake ya soka. Solskjaer anaweza kufufua kiwango chake akiwa Besiktas.
Victor Lindelof, beki wa kati wa Sweden mwenye miaka 31, hajapata nafasi Manchester United na mkataba wake unakamilika msimu huu. Solskjaer anaweza kumshawishi kujiunga na Besiktas badala ya kwenda Leicester.
Christian Eriksen, kiungo wa Denmark mwenye miaka 32, ameanza kuhusishwa na klabu kama Celtic, lakini Besiktas wanaweza kuwa chaguo jingine kwa kiungo huyo mwenye uzoefu.
Antony, winga wa Brazil, ameshindwa kung’aa Old Trafford tangu ajiunge kwa pesa nyingi. Besiktas wanaweza kumchukua kwa mkopo, ingawa Real Betis pia wanamtaka.
Casemiro, kiungo wa zamani wa Real Madrid, ameanza kuhusishwa na Ligi ya Saudi Arabia, lakini angefaa katika ligi ya Uturuki. Changamoto kubwa inaweza kuwa mshahara wake mkubwa, lakini bado anaweza kuwa nyongeza bora kwa Besiktas.
Solskjaer anakabiliwa na changamoto kubwa, lakini wachezaji hao wanaweza kumsaidia kubadilisha hali ya Besiktas na kutokana na uhusiano uliopo kati ya Solskjaer na Manchester United, basi ana uwezekano wa kunasa saini za wachezaji hao

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button