Kwingineko

PSG, Bayern viwanja tofauti UCL

PARIS Saint-Germain na Bayern Munich leo zinashuka kwenye viwanja tofauti katika michezo ya marudiano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UCL) hatua ya 16 bora.

PSG itakuwa ugenini kuikabili Real Sociedad kwenye uwanja wa Reale uliopo mji wa San Sebastián, Hispania. Katika mchezo wa kwanza PSG ilishinda kwa mabao 2-0.

Bayern Munich itakuwa uwanja wa nyumbani wa Allianz katika jiji la München, Ujerumani kuikaribisha Lazio ya Italia. Lazio ilishinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.

Related Articles

Back to top button