Ligi Kuu

Simba yawaonya wachezaji wa Pamba Jiji FC

MWANZA: KUELEKEA kwenye mchezo wa leo Ligi Kuu Bara, Pamba dhidi ya Simba, uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo huo umekamilika na wanahitaji alama tatu.

Amesema wachezaji waliopo kwenye majukumu ya timu za Taifa, akiwemo Mohammed Hussein  Shomari Kapombe, Kibu Denis, Aishi Manula kutoka Stars na Moussa Camara (Guinea) wamerejea na kuendelea na maandalizi dhidi ya Pamba Jiji FC. Amesema Steven Mukwala amekwenda moja kwa moja Mwanza kuungana na kikosi kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya timu hiyo kutafuta  pointi tatu ugenini.

“Ratiba ya mechi za kalenda ya fifa haijaharibu maandalizi kuelekea mchezo wetu wa kesho, wachezaji wengi wametumika kwwnye timu zao za Taifa, hivyo wapo timamu kimwili na wapo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Pamba,” amesema.

Katika hatua nyingine uongozi wa Simba umewaomba wachezaji pinzani kuacha kucheza vibaya na kuwaparamia wachezaji wao. Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba,  Ahmed Ally amesema baada ya mechi ya Pamba Jiji FC wanajukumu kubwa la kupambania Simba katika mchezo wa kimataifa.

Amesema wachezaji wa Pamba kucheza bila kufuata maelekezo ya kusababisha wachezaji wao kupata majeraha ya lazima kwa sababu wanaimani utakuwa mchezo mzuri.

“Tunawaomba wachezaji wa Pamba waje wacheze mpira, wasije kucheza kwa kupania, wasije kucheza kwa kukamia, wakawaumiza wachezaji wetu wasicheze kwa nia ovu wachezaji washindwe kucheza mechi za kimataifa.

“Bado tunakumbuka yaliyotokea kwa kijana wetu Moses Phiri alivurugwa kabisa kijana wetu kwenye maisha yake ya mpira hivyo tunawaomba waamuzi waliangalie hili kwa umakini.” Ahmed.

Related Articles

Back to top button