Ligi KuuNyumbaniTetesi

Man City kumsajili Sávio

TETESI za usajili zinasema Manchester City imekubali dili kumsajili winga wa Brazil, Sávio Moreira de Oliveira, maarufu Sávio, ambaye kwa sasa yupo Girona ya Hispania kwa mkopo majira yajayo ya kiangazi, toka klabu ya Troyes ya Ufaransa.

Girona na Troyes ni sehemu ya City Football Group.(Fabrizio Romano)

Barcelona imepokea ofa toka Tottenham ya jumla ya Euro mil 70 kwa ajili ya kumsajili Raphinha huku Spurs ikikusudia kulipa ada maalum ya Euro mil 58 kwa ajili ya winga huyo. (SPORT – Spain)

Real Madrid haijakubaliana vipengele binafsi na Kylian Mbappé kuhusu uhamisho huru unaotarajiwa toka Paris Saint-Germain majira yajayo ya kiangazi. (Independent)

Mbali na Mbappé, Real Madrid pia ina nia kumsajili Bruno Guimaraes toka Newcastle. Chelsea na Liverpool pia zinamwinda kiungo huyo.(Fichajes – Spain)

Fowadi wa Bayern Munich, Leroy Sane hafikirii uhamisho majira ya kiangazi kwenda Barcelona, ingawa hajafunga mlango uwezekano wa kurejea Ligi Kuu England kufuatia nia ya Liverpool kumsajili.(SPORT – pain)

Related Articles

Back to top button