Ligi Kuu

Simba yatamba kumpata mrithi wa Chama

DAR ES SALAAM: UONGOZI wa klabu ya Simba umefanikiwa kumpata mbadala wa Clatous Chama, Ahoua Jean Charles kwa mkataba wa miaka miwili kutumikia kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi.

Simba inaendelea kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa kumtambulisha kiungo mshambuliaji Ahoua Jean Charles anayesajiliwa akitokea klabu ya Stella dead James ya nchini Ivory Coast akija kuchukuwa nafasi ya Chama aliyejiunga na Yanga.

Ahoua ameibuka mchezaj bora nchini humo na klabu yake akifunga mabao 12 na kutoa pasi za mwisho ‘Assist ‘, tisa katika ligi ya Ivory Coast.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wamefanikiwa kumnasa kiungo huyo ambaye anauwezo mzuri na kutegemea mambo makubwa kwa kushirikiana na nyota wengine na wale waliopo kikosini.

Amesema anasifika kwa kufunga mabao kutoka umbali mrefu kuchezesha timu pamoja na kutengeneza nafasi kwa wenzake.

“Tumemfatilia uwezo wake anauwezo wa kuchezesha timu, ikiwa anafanya kazi aliyokuwa akiifanya Chama hatuna presha wala hofu juu ya kuwa ni mbadala wake ndani ya kikosi cha Simba,” amesema Ahmed.

Amesema suala la usajili linaendelea kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo kuboresha kila eneo lenye mapungufu na kutegemeza timu imara ya msimu ujao.

 

Related Articles

Back to top button