Ligi KuuNyumbani

Simba yashusha mwingine

 

KLABU ya Simba imetangaza kukamilisha usajili wa Kiungo Abdallah Hamisi kwa kandarasi ya miaka miwili.

Nyota huyo wa zamani wa timu za Muhoroni Youth Fc, Bandari Fc na Sony Sugar za Kenya amejiunga na Simba akiwa mchezaji huru.

Kupitia kurasa za mitandao za timu hiyo imechapishwa taarifa ya kuinasa saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania.

Mchezaji huyo anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa leo Julai 20, 2023 baada ya mapema leo Shabani Iddi Chilunda kutambulishwa msimbazi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button