Ligi Kuu

Gamondi: Chama, Pacome, Aziz Ki niachieni mimi

Kocha wa Yanga Miguel Gamondi kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu usajili mpya unaoendelea kufanywa ndani ya timu hiyo.

Jana kocha huyo alifungua rasmi maandalizi ya msimu mpya na kukutana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo.

Baada ya mazoezi ya siku ya jana Master ‘Gamondi’ amesema amefurahishwa na usajili uliofanywa kwani utampa machaguzi mengi kikosini.

“Tuna michezo mingi sana mfano msimu uliopita tulikuwa na michezo zaidi ya 50 nadhani unapokuwa na wachezaji wengi wenye ubora unakuwa na machaguo mengi , huyu anaweza kutokea benchi na kuja kubadilisha mchezo” amesema Gamondi

Kiu ya mashabiki wa Yanga ilikuwa ni kujua jinsi kocha huyo atakavyowatumia viungo Aziz Ki, Pacome Zouzoua na Clatuos Chama na majibu ya Gamondi ni kwamba hakuna shinikizo lolote kwake kwani kila mmoja tapata nafasi kuendana na aina ya mchezo.

Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji watano na kuwaongezea wengine mkataba na tayari wameanza rasmi maandalizi ya msimu mpya huku wakidhamiria kufanya kweli kwenye michuano watakayoshiriki msimu ujao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button