Mzize: Bado hamjasema nitawafunga sana!
DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize ameweka wazi kuwa akitokea benchi huwa anafanya vizuri zaidi kuliko anapoanza ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo .
Amesema mara nyingi anapokuwa benchi huwa anaangalia mapungufu ya mabeki wa timu pinzani na kuingia kuwaadhibu kwa kufunga au kuwasumbua wapinzani .
Mshambuliaji huyo amesema akianzia benchi huwa anausoma vizuri mchezo na kuingia kusahihisha makosa ya wenzake huku akitamba kuwa wapinzani kazi wanayo msimu huu.
‘Mwaka huu nimekuja kivingine akili imekuwa tofauti na msimu uliopita, kwa kuwa akili ilikuwa ya kitoto na kuathiriwa na maneno ya mashabiki mtandaoni., amesema Mzize na kuongeza
“Nikicheza pembeni inakuwa nzuri zaidi kwasababu akili yangu inawaza kufunga zaidi hasa nikicheza namba saba ni rahisi kwa kuwa natumia kushoto,” amesema Mzize.