Ligi KuuNyumbani

Ihefu kuendeleza ushindi leo?

BAADA ya Ihefu kuhitimiza safari ya Yanga kutofungwa michezo 49 ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ushindi wa mabao 2-1 timu hiyo ya Mbarali mkoani Mbeya leo ni mgeni wa Kagera Sugar katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Ihefu ipo nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 14 wakati Kagera Sugar ni ya 9 ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 13.

Mchezo mwingine wa ligi kuu leo utashuhudia Singida Big Stars ikiwa mwenyeji wa Namungo kwenye uwanja wa Liti mjini Singida.

Singida Big Stars inashika nafasi 4 ikiwa na pointi 24 baada ya michezo 13 wakati Namungo ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 13.

Related Articles

Back to top button