Africa

Simba yaishika Yanga pabaya, inauma!

DAR ES SALAAM: SIMBA imeamua kupiga kwenye mshono baada kumtangaza kiungo, Yusuph Kagoma kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya.

Kagoma amekuwa gumzo baada ya Yanga kudai kuwa ni mchezaji wao halali na kupeleka pingamizi kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini TFF kuwa nyota huyo wamemsajili kwa kufanya makubaliano na timu yake ya zamani ya Fountain Gate FC.

Simba tayari imerejea nchini ikitokea Libya na kuingia kambini kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly Tripoli, Jumapili, Septemba 22 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam..

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema ikiwa ni desturi ya klabu hiyo kuwapa ugeni rasmi wachezaji au benchi la ufundi katika michezo ya kimataifa wanapocheza nyumbani.

“Mechi yetu hii ya Jumapili, mgeni wetu rasmi atakuwa Kagoma, mchezaji wetu na ameonyesha kiwango kizuri mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Libya, kulingana na ubora huu aliounesha tunalazimika kumpa heshima hiyo,” amesema Ahmed.

“Tumerudisha viingilio vya kawaida kuanzia elfu 3000 hadi 5000, kwa sababu sio mechi ya faida bali tunahitaji kupata matokeo ya ushindi na wanasimba wapate nafasi ya kwenda kwa wingi uwanjani kuipeleka Simba makundi.

Huu mchezo upo 50 kwa 50, atakayechanga karata zake vizuri ndio anayeenda makundi, Simba wanafaida kubwa ya kuingia makundi kwa kutumia mashabiki wetu tuingie kwa wingi uwanjani,” amesema Ahmed.

“Hatudharau mashindano yoyote, itakuwa fedheha kubwa tutakaposhindwa kufuzu makundi na tena nyumbani. Mechi ya Libya ilikuwa jukumu la wachezaji na benchi la ufundi na wamefanikiwa kupata sare, mechi hii ni ya Wanasimba wote tushikamane na tuwe pamoja kuhakikisha Simba inafuzu hatua ya makundi,” amesema meneja huyo.

Ameongeza kuwa licha ya kutoka suluhu lakini Al Ahly Tripoli wamewafunga mabao 2-0 wa nje ya uwanja, ikiwemo mashabiki elfu 50, wanahitaji kusawazisha hilo kujitokeza kwa wingi na kuujaza  uwanja na bao pili  mashabiki wao kuvaa jezi zao, ukinagalia kila mmoja alivaa jezi ya klabu hiyo,  hilo tunawajibu la kusawazisha Septemba 22, kwa kuvaa jezi yake ya Simba ikiwezekana mpya ya msimu wa huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button