Ligi Kuu

Simba Vs Yanga hakuna ‘umeme’

JUMAMOSI Oktoba 19 ni Kariakoo Dabi, Simba ikiialika Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu raundi ya kwanza machinjioni Benjamini Mkapa.

Kuelekea mchezo huo leo tunakusogezea baadhi ya mambo muhimu kuhusu timu, makocha na wachezaji waliowahi kucheza au wanacheza mpaka sasa kwenye klabu za Simba na Yanga.

Je unafahamu kwamba tangu mwaka 2020 hakuna mchezaji aliyepata kadi nyekundu katika mchezo uliozikutanisha timu hizo katika ligi kuu?.Ndio tangu mwaka huo licha ya ugumu wa mchezo huo hakuna mchezaji aliyekula ‘umeme’ ila mchezo huo umetawaliwa na kadi nyingi za njano.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wenye kadi nyingi zaidi za njano kwenye michezo uliozikutanisha timu hizo tangu mwaka 2020.
Nyota wa zamani wa Yanga, Feisal Salum anaongoza akiwa na kadi 4 huku mlinzi wa zamani wa Simba Joash Onyango akifuatia na kadi tatu sawia na nahodha msaidizi wa Yanga Dickson Job pamoja na kiungo Jonas Mkude.

Clatous Chama wa Yanga ana kadi mbili za njano kama ilivyo kwa nahodha wa Simba Mohamed Hussein, Stephane Aziz Ki(Yanga), Khalid Aucho( Yanga) Mzamiru Yassin( Simba) Bernad Morrison na Djuma Shabani.

Jumamosi mashabiki wanakwenda kushuhudia kwa mara nyingine ubabe wa miamba hii ya soka la Tanzania, imezoeleka siku ya Kariakoo Dabi ni zaidi ya sikukuu kwa mashabiki wa timu hizo pendwa nchini, kuzodoana na vijembe ni mambo ya kawaida katika juma lililobeba dabi.

Related Articles

Back to top button