
KAIMU Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda amesema atahakikisha kikosi chake kinabeba pointi zote 18 katika mechi sita za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara itakazocheza timu hiyo Novemba.
Akizumgumza na Spotileo, kocha huyo amesema anatambua haitakuwa kazi rahisi kutokana na ushindani uliopo lakini yeye na wachezaji wake wamejipanga kuhakikisha lengo hilo linatimia.
“Natambua ugumu uliopo kwenye ligi lakini lazima kupambana na ushindani uliopo ili kutimiza lengo letu ambalo ni ubingwa,” amesema Mgunda.
Amesema kabla ya ubingwa wanataka kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa wanaongoza ligi.
Mechi sita za Simba Novemba ni dhidi ya Singida Big Stars, Ihefu, Namungo, Ruvu Shooting, Mbeya City na Polisi Tanzania.