Ligi KuuNyumbani

Simba kuanza kampeni Ligi Kuu leo

MIAMBA ya soka nchini Simba, leo inaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo pekee leo wa ligi hiyo utafanyika kwenye uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoa wa Morogoro.

Ligi hiyo imeshuhudia michezo miwili Agosti 16, Azam ikiifunga Tabora United mabao 4-0 na Mashujaa ikiichapa Kagera Sugar mabao 2-0.

Hata hivyo, mchezo wa Azam na Tabora United ulishindwa kuendelea baada ya wachezaji wawili wa Tabora UTD kuumia na kufanya wabakie sita uwanjani na hivyo mchezo kukosa sifa kikanuni kuendelea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button