Filamu

Shamsa Ford ajitapa na ndoa yake

MREMBO Shamsa Ford amesema kuwa hayupo tayari kuwa mke wa pili wa mume wake,Hussein Lugendo,anayefahamika kama Mulilo.

Shamsa amesema endapo mwanamke yeyote akifuatwa na mume wake ,basi ajue kabisa anadanganywa kwani yeye ndio mwenye nyumba na yuko peke yake.

“Mume wangu ananipenda,ni mtulivu na hana mtu mwingine zaidi yangu.Kwake niko peke yangu,ninajiamini kwa sababu napendwa.”

“Mwanaume anaongeza mke mwingine kwa mkwa sababu fulani aidha mwanamke jeuri, hawezi kumshauri mumewe hata jambo la maana hata siku moja, na kukiwa hakuna maendeleo,hapo ni lazima atakuongezea mwenzako. Kama wanavyosema Mwanamke jeuri mwongezee mwenzie”,amesema Shamsa.

Akazidi kusema”hata siku moja haitatokea, yaani ikitokea nimefanya kosa lolote basi nitamruhusu mume wangu kuoa mke wa pili, lakini kwasasa naona hakuna sababu ya mume wangu kuoa mke wa pili kwa kuwa nipo vizuri na ninajitosheleza kila idara.”

Pia ameongeza kuwa kikubwa anachojivunia kwa mumewe ni heshima,usikivu,vitu ambavyo ndio Siri kubwa ya ndoa yao kudumu.

Related Articles

Back to top button