“Serikali isipolinda Tasnia, Filamu za Kihindi zitaporomoka”

MUMBAI: MUONGOZAJI wa filamu Vivek Agnihotri, anayesifika kwa kutengeneza filamu ya ‘The Kashmir Files’, ‘The Tashkent Files’ na nyingine nyingi, ameitaka serikali ya India kulinda tasnia ya filamu za Kihindi dhidi ya kuporomoka.
Muongozaji huyo wa filamu amesema kuwa kuna maswala mengi katika tasnia ya filamu za Kihindi ambayo watu binafsi na vyama havitaweza kuyatatua.
Vivek Agnihotri pia ameandika barua ya wazi kwa Waziri wa Biashara na Viwanda Piyush Goyal kuhusu jambo hilo.
Vivek Agnihotri amesema anataka serikali isaidie tasnia ya filamu za Kihindi ifufuke kwani sinema hizo zinatatizika katika sekta ya maonesho.
Amesema; “Tasnia hii ya filamu ya Kihindi inaporomoka. Kuna mambo mengi, na sio ya kulaumu mtu yeyote. Lakini nyakati zimebadilika, na teknolojia imebadilika, jinsi watu wanavyotumia sinema pia imebadilika. Kuna shida kubwa, na sidhani mtu yeyote au chama kinaweza kutatua zaidi ya serikali ya India.
Muigizaji wa filamu alitoa mfano wa tasnia za filamu katika nchi kama Ufaransa, Uingereza na Korea Kusini ambapo biashara ya maonesho inalindwa na serikali zao.
“Kile ambacho Ufaransa imefanya barani Ulaya ni kwamba waligundua kuwa sinema sio sanaa tu, lakini inaweza kuwa tasnia yenye nguvu sana na nguvu laini. Kwa hivyo waliilinda. Kama Uingereza ilifanya Tume ya Filamu ya Uingereza,
Nchi zote za Ulaya zina tume hizi. Serikali ya Korea inaunga mkono K-burudani, na serikali ya China inaunga mkono filamu zao. Nchini Japan, jamii inaunga mkono sinema kwa njia kubwa sana.” Ameeleza.
Muongozaji huyo pia amesikitishwa na kiwango kikubwa kinachotozwa kwa wadau wa filamu anapokwenda kutazama filamu katika majumba ya sinema nchini humo akidai wenzao wa kusini wanachaji nafuu hivyo wadau wengi hukimbilia huko na kukicha majumba ya sinema na mijini huku akidai wengi wao wanatazama kwenye OTT badala ya kumbi za sinema.
Kwa mujibu wa muongozaji huyo, biashara ya filamu huathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na sababu zilizotajwa. Hivyo, anatarajia kuungwa mkono na serikali ya India.