Patcho Mwamba, Uwoya kuonesha tamthilia mpya
TAMTHILIA ya Mzani wa Mapenzi iliyochezwa na wasanii Irene Uwoya, Miriam Ismaili na Patcho Mwamba kuanza kuruka rasmi Agosti 23, 2023 chaneli ya Sinema zetu baada ya kuaga Toboatobo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tamthilia hiyo jijini Dar es Salaam Msimanizi Mkuu wa Sinema zetu Sophia Mgaza amesema tamthilia ya Mzani wa Mapenzi inakuja ndani ya sura nyingine katika kitovu cha jiji la kibiashara la Dar es Salaam ikiwa na mandhari ya kuvutia na maeneo mengi ya kitalii.
“Azam imewasogeza sebuleni kwako wakali wa fani hii kwa pamoja wakiwa ndani ya tamthilia ya Mzani wa Mapenzi Irene Uwoya na Patcho Mwamba baada ya ukimya wao wanaokuja kwa sura nyingine ndani ya tamthilia hii iliyozalishwa Jijini hapa kupitia maandhari za kuvutia na maeneo mengi ya kitalii katika ufuo wa Bandari Salama yakitumuka kuipamba tamthilia hii” Amesema Mgaza.
Ameongeza kuwa Mzani wa Mapenzi ni tamthilia inayozungumzia wanandoa wenye mitazamo na matamanio tofauti juu ya furaha zao ambapo Cecy anawakilisha kundi la wale wenye kuamini kuwa ndoa ni tunu inayohitaji kulindwa huku mumewe victor akijiridhisha kuwa mwanaume barubaru katika katika ndoa ni yule mwenye walau Mpango wa Kando.
Amesema tamthilia hiyo imesheheni wasanii mahiri na chipukizi akiwemo Marium Ismail kama Cecy, Sharon Kabwita kama Kai, Irene Uwoya kama Cleopatra, Habibu Mtambo kama Victor, Alex Mgeta kama Alex, Marium Fereji kama Mercy, Lightness Lodvick kama Peace, Patcho Mwamba kama Bruno na Fredy Kiluswa kama Dr.Maja.
“Lengo la Azam Media LTD ni kuendelea kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamaji wetu huku tukisukuma sanaa yetu kimataifa, hasa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na popote ambapo AzamTVMax inaweza kufika” Amesisitiza Mgaza.
Kwa upande wake Alex Mgeta amesema kuwa tamthilia ya Mzani wa Mapenzi itakuwa tiba kwa wale wanaosumbuliwa na mapenzi.