Habari Mpya

Sanaa na Utamaduni Kuitangaza Tanzania Nchini India

HARYANA:BALOZI wa Tanzania nchini India, Anisa Mbega, ameahidi kuendelea kupanua fursa kwa vikundi vya sanaa na utamaduni kushiriki katika maonesho mbalimbali nchini India ili kukuza soko la bidhaa na ubunifu wao.

Akizungumza alipotembelea banda la Tanzania katika Maonesho ya 38 ya Surajkund Crafts Mela yaliyofanyika Haryana, India, Balozi Mbega alisema kuwa ushiriki wa wasanii na wajasiriamali kwenye matukio kama haya unachangia kuongeza mwonekano wa Tanzania kimataifa.

Katika maonesho hayo, wajasiriamali wa Kitanzania waliuza bidhaa mbalimbali za asili, huku kikundi cha ngoma cha Magoma Moto kutoka Bagamoyo kikiburudisha hadhira na kuonesha utajiri wa utamaduni wa Tanzania.

Maonesho ya Surajkund Crafts Mela, yanayoshirikisha zaidi ya nchi 50, yalianza Februari 7 na kufikia tamati Februari 23, 2025. Hufanyika kila mwaka na yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kutangaza sanaa, utamaduni, na biashara za nchi shiriki.

Related Articles

Back to top button