Simba yaambulia nafasi ya tatu
DAR ES SALAAM: SIMBA imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika michuano ya timu nne ya ngao jamii baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union leo uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Simba limefungwa na nyota Salehe Karabaka dakika ya 10 kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Simba imecheza mchezo wa mshindi wa tatu baada kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa nusu fainali alhamisi iliyopita wakati Coastal Union akipoteza mbele ya Azam FC.
Katika mchezo wa mshindi wa tatu timu hizo zilionyesha uwezo mkubwa hadi Dakika 45 kipindi cha kwanza kimekamilika Simba 1-0 dhidi ya Coastal Union, timu zote zilifanya mashambulizi kwa zamu kila timu ikifika golini kwa mwenzake na kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.
Kikosi cha Simba: Moussa Camara, Kelvin Kijili, Mohammed Hussein, Abdulrazack Hamza, Che Malone Fondoh, Agustino Okejepha, Salehe Karabaka, Debora Fernandes, Steven Mukwala, Jean Ahoua na Joshua Mutale.
Coastal Union: Chuma Ramadhani, Jackson Shija, Miraji Hassan , Mukrim Issa, Abdallah Dennis, Semfuko Daud, Denis Modzaka, Ramadhani Iddi, John Makwata, Lucas Kikoti na Hernest Malinga.