Habari Mpya

BASATA na Tanzania Bora Initiative wajadili mustakabali wa sanaa nchini

DAR ES SALAAM:Katika mkutano uliofanyika jana, Februari 25, 2025, Katibu Mtendaji wa BASATA, Dk. Kedmon Mapana, amekutana na viongozi wa taasisi ya Tanzania Bora Initiative katika Jumba la Makumbusho, Posta – Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha sekta ya sanaa nchini na kuboresha mazingira ya kazi kwa wasanii wa Kitanzania.

Katika kikao hicho, pande zote mbili zilijadili changamoto zinazoikabili tasnia ya sanaa pamoja na fursa zilizopo.

Viongozi walijadili mikakati ya pamoja ya kuchochea ubunifu, kuongeza ajira, na kukuza ukuaji wa sekta ya sanaa kama nyenzo muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Dkt. Mapana alisema kuwa ushirikiano huu unalenga kuunda mazingira yanayowahamasisha wasanii chipukizi na kuongeza uwekezaji katika tasnia ya sanaa, ambayo ina mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya jamii.

Majadiliano haya yanaashiria hatua chanya kuelekea mustakabali mzuri wa sanaa nchini Tanzania, ambapo taasisi mbalimbali zinashirikiana kuendeleza na kuboresha ubunifu, hivyo kuongeza thamani na umaarufu wa kitamaduni wa taifa.

Related Articles

Back to top button