La Liga

Rufaa ya Real Madrid yapigwa chini

MADRID, Rufaa ya kupinga kadi nyekundu aliyepewa kiungo wa Real Madrid Jude Bellingham katika mchezo dhidi ya Osasuna imekwaa kigingi baada ya kamati ya Waamuzi ya shirikisho la soka nchini Hispania (CTA) kuitupilia mbali.

Real Madrid walikata rufaa kupinga adhabu ya Bellingham kufungiwa mechi mbili kufuatia kadi nyekundu aliyopata kwa kile kinachotajwa kuwa ni lugha chafu dhidi ya mwamuzi huyo kwenye mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1

Kufuatia kushindwa huku sasa Jude Bellingham atakosa michezo miwili ya Laliga dhidi ya Girona wikiendi hii na dhidi ya Real Betis kukosekana kwake kunaongeza uchungu kutokana na ugumu wa ratiba ambao kocha wake Ancelotti amekuwa akilia mara nyingi.

Related Articles

Back to top button