Rosa Ree aumizwa na kinachoendelea Goma

DAR ES SALAAM: RAPA Rosary Robert ‘Rosa Ree’ amesema kinachoendelea Goma kule Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kinaumiza sana.
Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Instagram, nyota huyo ameandika ujumbe akiwalilia madereva watanzania waliokwama kule kwasababu ya vita vinavyoendelea.
Rosa Ree ameweka video ya madereva wanaoomba msaada na kusema: “Kwa muda mrefu nashindwa hata kutoa ngoma mpya maana nikiangalia dunia ilipofika sasa hivi moyo unajaa majonzi,
“Mauaji yamekua kawaida, mabaya yameanza kuonekana mazuri na mazuri yanaonekana ushamba, wanaume wameanza kuwa wanawake, wanawake kuwa wanaume, kizazi cha kesho kinajifunza nini? Na sisi wasanii tutafumba macho na kuimba nyimbo za mapenzi tukiwaza valentine?”
“Tutaendelea kufanya ‘dance challenges’ kweli kama hatuoni yanayoendelea Afrika na duniani sasahivi???? Eh Mwenyezi Mungu ingilia kati turehemu sisi pamoja na vizazi vyetu,”