Mastaa

Jay-Z adaiwa kubaka

Aunganishwa kesi ya P.Diddy

NEW YORK: KESI iliyorekebishwa na kuwasilishwa katika mahakama ya shirikisho wikiendi hii inadai kwamba msanii maarufu wa rap Jay-Z alimbaka msichana wa miaka 13 pamoja na Sean ‘Diddy’ Combs wakati wa tafrija mwaka wa 2000.

Jay-Z amekanusha madai hayo kwenye mitandao ya kijamii na akakashifu kesi hiyo, akiitaja kuwa ni sehemu ya ‘jaribio la uwongo’.

Wanasheria wa Jay-Z hawakujibu mara moja ombi la maoni hayo.

Kesi hiyo iliwasilishwa mwezi Oktoba katika Wilaya ya Kusini ya New York na wakati huo haikumtaja Jay-Z kama mshtakiwa, ingawa kesi iliyorekebishwa inasema kwamba Jay-Z alitambuliwa kama ‘Mtu Mashuhuri A’ kwenye malalamiko ya awali.

Combs amekanusha tuhuma zote dhidi yake, ikiwa ni pamoja na hii, mwezi Oktoba. Kwa sasa yuko jela kwa mashtaka ya ulanguzi wa ngono ya shirikisho, ambayo amekana.

Kesi hiyo inadai kuwa msichana huyo ambaye hakutajwa jina alilewa na kubakwa na Jay-Z na Combs kwenye tafrija iliyoandaliwa na Combs kufuatia Tuzo za Muziki za MTV mnamo 2000, zilizofanyika New York.

Tony Buzbee, wakili wa Texas anayewakilisha msichana ambaye alifungua kesi siku ya Jumapili, amewasilisha mashtaka ya kiraia angalau 20 dhidi ya Combs akimtuhumu kwa utovu wa nidhamu wa kijinsia.

Katika barua pepe kwa Reuters, Buzbee amesema kesi ya Jay-Z ‘inazungumza yenyewe.’

“Hili ni suala zito sana ambalo litafikishwa mahakamani,” Buzbee ameandika.

Buzbee, katika kesi yake iliyorekebishwa, anasema kampuni yake ya kisheria hapo awali ilikuwa imemtumia Jay-Z barua ya kutaka kupatanisha suluhu.

Jay-Z, kesi hiyo inasema, alijibu barua hiyo kwa kufungua kesi dhidi ya Buzbee, na kwa ‘kupanga njama ya unyanyasaji’ dhidi ya Buzbee na mawakili wengine katika kampuni yake, ambayo wakili huyo amesema ilikuwa mbinu ya vitisho iliyokusudiwa kumnyamazisha mteja wake.

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii, Buzbee amesema mhasiriwa anayedaiwa kubakwa anayemwakilisha “hakuwahi kudai hata senti” kutoka kwa Jay-Z, akiandika kwamba, alitafuta tu upatanishi wa siri.”

Buzbee wiki iliyopita alifungua kesi dhidi ya kampuni ya mawakili ya Quinn Emanuel Urquhart & Sullivan, ambayo mawakili wake wanawawakilisha Combs na Jay-Z, akishutumu timu ya wanasheria wa kampuni hiyo kwa kuwanyanyasa wafanyakazi wenzake, wateja wake na familia yake.

Related Articles

Back to top button