Rooney aionya England mchezo dhidi ya Marekani
Mkongwe wa soka wa England ambaye pia ni Kocha wa klabu ya D.C United anaamini timu ya taifa ya Marekani ina nafasi kuiduwaza England leo baada ya kuziona timu hizo zilivyocheza mechi za ufunguzi za michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Qatar.
Rooney amesema England inahitaji kuwa makini kuanzia mwanzo wa mchezo vinginevyo inaweza kuduwazwa.
“Marekani watafanya mashambulizi eneo la England na utakuwa mchezo wenye changamoto tofauti kabisa na ule England iliyocheza dhidi ya Iran. Ni mchezo mgumu,” amesema Rooney
Amewataja baadhi ya wachezaji bora wa kikosi cha Marekani kuwa ni pamoja Christian Pulisic, Weston McKennie, Yunus Musah, Brenden Aaronson na Tyler Adams.
Katika michezo ya ufunguzi kundi B Novemba 21 England iliichapa Iran mabao 6-2 huku Wales na Marekani zikitoka sare ya bao 1-1.




