World Cup

AI yatumika mpira wa CWC

MAREKANI: KAMPUNI ya vifaa vya michezo ya Adidas na FIFA wamezindua rasmi mpira utakaotumika katika mashindano ya kombe la dunia la klabu yatakayofanyika Juni mwaka huu nchini Marekani mpira ambao wameutengeneza kwa usaidizi mkubwa wa akili bandia (Artificial Intelligence) AI.

Mpira huo umejichotea rangi zake kutoka kwenye bendera ya Marekani ambaye ni mwenyeji wa kwanza wa michuano hiyo ambayo inakuja na sura mpya na umetawaliwa kwa kiasi kikubwa na rangi nyekundu, nyeupe na bluu huku ukiwa na nakshi za rangi ya dhahabu.

Zaidi mpira huo unakuja na teknolojia ya kipekee itakayounganishwa na mfumo wa VAR ili kurahisisha utumaji wa taarifa za mchezo na kusaidia maamuzi. Teknolojia hiyo pia inategemewa kuondoa utata hasa katika matukio ya offside na mpira kuchezwa kwa mkono.

Mpira huo pia umetengenezwa kwa malighafi itakayoufanya uwe mwepesi hivyo kufanya uwe na kasi na rahisi hivyo kupunguza adha kwa wachezaji

Timu kutoka Ulaya, Afrika, Asia Australia Amerika ya Kusini na kaskazini zitaoneshana umwamba kwenye michuano hiyo itakayoanza Jumamosi ya Juni 14, 2025

Related Articles

Back to top button