Ronaldo amuenzi Jota baada ya ushindi dhidi ya Croatia

TORONTO:BAADA ya kuiongoza Ureno kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Croatia na kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia, Cristiano Ronaldo alitoa heshima maalumu kwa aliyekuwa mchezaji mwenzake, Diogo Jota.
Mara baada ya mchezo kumalizika, Ronaldo alivaa jezi ya timu ya taifa ya Ureno yenye namba 21, namba aliyokuwa akiitumia Diogo Jota.

Tukio hilo lilikuwa la kugusa hisia za wengi, kwani lilifanyika siku ambayo ilitimiza mwaka mmoja tangu kifo cha Jota, ambaye alifariki na kuacha majonzi makubwa kwa familia yake, wachezaji wenzake na mashabiki wa soka duniani.
Kwa kitendo hicho, Ronaldo alionesha kuwa licha ya ushindi muhimu walioupata, bado hawajamsahau mwenzao ambaye aliwahi kulitumikia taifa lao kwa moyo wote.
Ilikuwa ni heshima ya kimya lakini yenye ujumbe mkubwa, huku wengi wakiamini kuwa ushindi huo ulipewa maana ya kipekee kwa kumbukumbu ya Diogo Jota.





