Kwingineko

Arsenal kupindua meza kibabe?

KOCHA wa washika mitutu wa jiji la London Arsenal Mikel Arteta amesema hawana chaguo lingine bali kuingia kwa nguvu zote kwenye mchezo wa kombe la Ligi ‘Carabao Cup dhidi ya Newcastle United leo katika dimba la St James Park.
Arteta amewaambia waandishi wa habari kuelekea mchezo huo kuwa ikiwa wanataka kusonga mbele ni lazima wajitume na wachezaji wajitoe kwa nguvu zote kuhakikisha wanapata ushindi wa jumla utakaowawezesha kucheza fainali ya kombe hilo.

“Tunataka kuipambania nafasi hii, tuna morali inayotokana na matokeo mazuri ya mechi zetu za karibuni,tutaingia kwa nguvu ni lazima tufanye hivyo kama tunataka kushinda kama tunataka kufika fainali” Amesema.

Tunajua sio timu rahisi hata kidogo tuliwafunga mchezo wa nyumbani kwao msimu uliopita lakini msimu huu wamekuwa tofauti” – ameongeza

Mchezo huu ni wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza Arsenal kupotea nyumbani Emirates stadium kwa mabao 2-0. Na watakuwa na kibarua kizito cha kuishinda Newcastle United walio kwenye form nzuri msimu huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button