EPLTetesi

Chelsea yavuta waya kwa Enzo Maresca

Wababe wa Magharibi mwa jiji la London Chelsea the Blues wameonesha nia ya kuanzisha mazungumzo na mkufunzi wa Leicester City Enzo Maresca kama mthirthi wa Mauricio Pochettino aliyeondoka klabuni hapo.

Maresca ameiongoza Leicester City kurejea Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza huku wasifu wake ukionesha hapo awali alifanya kazi Manchester City kama msaidizi wa Pep Guardiola.

Chelsea inatafuta Kocha mkuu mpya ambaye ataendana na mfumo wa klabu hiyo wa kucheza soka la kumiliki mpira, mwenye ushirikiano na aliye tayari kukimbia mbio za farasi wawili wa ligi hiyo Pep Guardiola na Mikel Arteta.

Mmiliki mwenza wa klabu ya Chelsea Behdad Eghbali tayari yupo jijini London kusimamia mchakato wa kumteua kocha mkuu mpya huku mchakato huo ukiongozwa na wakurugenzi wenza wa michezo Paul Winstanley na Laurence Stewart

Related Articles

Back to top button