Tennis

Rehema ana balaa huyo!

DAR ES SALAAM: BINGWA wa Michuano ya Tennis ya Wheelchair Tanzania, Rehema Said ameendelea kuitangaza vyema Taifa baada ya kuchukua tuzo zaidi ya moja katika michuano minne tofauti kwenye mashindano ya ‘Plock Cup and Plock Open’ yaliyomalizika leo nchini Poland.

Maahindano hayo yaliyoanza kutimua vumbi Septemba 16 hadi 19. Rehema ni mwakilishi pekee katika mashindano hayo.

Rehema ameshika nafasi ya kwanza katika mchezo wa ‘Plock Cup single’ na nafasi ya pili ‘double wakiwa na mchezaji mwenzake Elizabeth William wa ‘USA’.

Katika hatua nyingine mchezo wa ‘Plock Open – Singles’ Rehema amepambana na kuishia hatua ya nusu fainali katika ‘Plock Open’ na fainali ya ‘doubles’ Rehema ameibuka mshindi wa pili kwa kuwashinda Zoya Chavdarova wa Bulgaria na Chiyo Sasaki wa Japan katika shindano la ‘IV PLOCK OPEN’ yanayoendelea nchini Poland.

Rehema anatarajia kurejea nchini Jumamosi Septemba 21, akiwa na mzigo wa kutosha wa tuzo alizopata katika michuano hiyo huku akitarajia kupokelewa na wadau wengi wamichezo nchini.

Related Articles

Back to top button