Djokovic atinga robo fainali Geneva Open
NYOTA wa mchezo wa tenisi Novak Djokovic ametia robo fainali ya michuano ya Geneva Open baada ya kumshinda mjerumani Yannick Hanfmann katika mchezo uliofanyika wakati wa kumbukumbu ya kutimiza miaka 37 na huku mvua ikinyesha.
Djokovic, bingwa mara 24 wa Grand Slam, anacheza mashindano ya ATP 250 huko Uswisi kwa mara ya kwanza ikiwa ni maandalizi ya michuano ya French Open na amemshinda mjerumani huyo kwa 6-3 6-3.
SOMA PIA: Carlos Alcaraz atinga robo fainali Miami Open
Ushindi huo umemfanya nyota uyo kuwa mchezaji wa tatu pekee baada ya Jimmy Connors na Roger Federer kushinda michezo 1,100 katika michuano ya ATP.
“Siku yangu ya kuzaliwa isingekuw ana aana iwapo nisingeshinda mchezo huu,” Djokovic amesema.
Novak Djokovic, anayeshika namba 1 kwa ubora duniani hafika fainali mwaka huu na hatua inayofuata atakabiliana na ama Denis Shapovalov wa Canada au Tallon Griekspoor wa Uholanzi.
Michuano ya French Open itaanza Mei 26 huku Djokovic akionekana kutetea taji lake na kushinda kwa mara nne.
Mashindano ya tenisi ya French Open maarufu Roland-Garros hufanyika kwa wiki mbili kila kwenye uwanja wa Roland-Garros katika mji mkuu wa Ufaransa Paris.
Mashindano na viwanja vinavyotumika zimepewa jina la Roland-Garros aliyekuwa ruani wa zamani.
Michuano mikubwa zaidi ya tenisi duniani ni Australian Open, French Open, Wimbledon na US Open.
Miongoni mwa michuano ATP hujumuisha ni pamoja na ATP Masters 1000, ATP 500, ATP 250, United Cup, ATP Challenger Tour, ATP Champions Tour for seniors, International Tennis Federation (ITF) Olympics, ATP Finals na Next Generation ATP Finals
Orodha ya wachezaji wa tenisi 10 bora duniani kwa mchezaji mmoja mmoja ni kama ifuatvyo:
1Novak Djokovic
2.Jannik Sinner
3.Carlos Alcaraz
4.Alexander Zverev
5.Daniil Medvedev
6.Andrey Rublev
7.Casper Ruud
8.Hubert Hurkacz
9.Stefanos Tsitsipas
10.Grigor Dimitrov
Kwa wachezaji wawili wawili bora duniani orodha ni kama ifuatavyo
1.Marcel Granollers
2.Horacio Zeballos
3.Matthew Ebden
4.Rohan Bopanna
5.Joe Salisbury
6.Rajeev Ram
7.Ivan Dodig
8.Austin Krajicek
9.Wesley Koolhof
10.Neal Skupski