Tennis

Tennis wasichana yajiweka sawa kuelekea Juni 10

DAR ES SALAAM. TIMU ya Taifa ya mchezo tenisi ya Wasichana inaendelea  na  mashindano ya Kombe la Billie Jean King yatakayofanyika Juni 10, mwaka huu nchini Rwanda.

Akizungumza na Spoti leo, Kocha wa timu hiyo, Nicolaus Leringa amesema, maandalizi yanaendelea vizuri, wachezaji wana morali ya kutosha kwa mashindano hayo.

Amesema amewaanda vizuri wachezaji hao ikiwemo kifundi na Kisaikolojia kuhakisha wanafanya kile ambacho wanakitarajia kwa kuipeperusha vema bendera ya nchini.

“Malengo ni kushinda kombe na kuipa nchi heshima, tupo tayari kupambania ushindi kwa kuwa haya ni mashindano makubwa,” amesema Leringa.

Ameongeza kuwa wanaenda kushindana katika mashindano hayo na sio kushiriki kwa sababu wanaimani kuwa na vijana wake kufuata maelekezo yote ambayo amewapa kipindi cha maandalizi ya mashindano hayo.

“Tumejipanga kuchukua kombe, kocha ameona madhaifu na kuyafanyia kazi nina imani mwaka huu tufanya vyema na kuliletea taifa heshima,” amesema Kocha huyo.

Wachezaji wanaunda timu hiyo ni Ester Namkulange, Emiliana Tarimo, Edna Mfinanga, Barbara Mollel na Edna John.

Related Articles

Back to top button