La Liga

Ramos popote kambi

KLABU yoyote inayohitaji saini ya beki Sergio Ramos itampata baada ya mkataba wake na Sevilla kumalizika na hivyo kuwa huru.

Ramos,38, alijiunga na klabu hiyo akitokea Paris Saint Germain ambako alifunga mabao manne ndani ya misimu miwili 2021-2023.

Mhispania huyo alijiunga na PSG akitokea Real Madrid ambako alijiunga 2005 akitokea Sevilla.

Taarifa za mtandao wa Salary Sports zinaonesha Ramos alikuwa akipokea £46,000 kwa wiki akiwa na klabu hiyo.

Hata hivyo zipo taarifa kuwa huenda Ramos akatimkia Saudia ambako kuna baadhi ya nyota aliowahi kucheza nao akiwemo Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.

Ramos alianza soka akiwa na klabu ya Camas mwaka 1991 na baadaye kwenda Sevilla, mwaka 2003 alijiunga na Sevilla, kabla ya 2005 kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Real Madrid.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button