La Liga

Barcelona wampa Yamal jezi yenye namba mpya

HISPANIA: WINGA wa Barcelona, Lamine Yamal, atavaa namba mpya ya jezi katika klabu hiyo kuanzia msimu wa 2024/2025.

Kwa mujibu wa uongozi wa timu hiyo, kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 atakabidhiwa jezi namba 19, ambayo ni namba sawa na anayovaa akiwa katika timu ya taifa ya Hispania.

Yamal alicheza msimu uliopita akiwa na usajili wa timu ya vijana na atapandishwa rasmi kwenye kikosi cha kwanza kabla ya kampeni ya 2024-25.

Hii itamaanisha nambari mpya ya jezi kwa kijana huyo, ambaye ameweka historia ya kutwaa kombe la Euro 2024 akiwa kijana mdogo tuna mwaka wa kwanza kuchezea timu ya taifa na kupata mafanikio makubwa.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu hiyo zimeeleza kwamba Yamal aliwekewa namba 19 na namba 10 akachagua jezi yenye namba 19 ndiyo anayotaka kuitumia akiwa katika timu ya wakubwa ya Barcelona.

Related Articles

Back to top button