Habari Mpya
Nyanda la boli lipo sana Jangwani
DAR ES SALAAM :RAIS wa Yanga, injinia Hersi Said amemtangaza kipa wao Djigui Diarra na kuweka wazi kuwa kipa huyo ameongeza mkataba wa miaka mitatu mingine kusalia ndani ya timu hiyo.
Diara alibakiza mkataba wa mwaka mmoja na ameongezewa miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya kikosi cha Kocha Miguel Gamondi kwa miaka mitatu tena.
Kipa huyo amesaidia Yanga kupata mafanikio kwa kutwaa mataji ya mashindano ya ndani kwa misimu mitatu mfululizo na timu hiyo kucheza fainali ya kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022/23.
Kwa msimu uliopita Diara alikuwa kwenye kikosi cha Yanga iliyovunja rekodi ya kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya zaidi ya miaka 20 kupita. Diara pia ndiye golikipa bora wa ligi kuu ya NBC msimu uliopita