Habari Mpya

Simba, Jobe ndo basi tena!

DAR ES SALAAM: KLABU ya Simba imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa mshambuliaji Pa Omary Jobe kwa kupindi kufupi cha miezi sita.

Jobe amejiunga na Simba katika dirisha la usajili wa mwezi Januari akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Zhenis inayoshiriki Ligi kuu nchini Zazakhstan.

Kuondoka kwa mshambuliaji huyo ni sehemu ya maboresho ya kikosi cha timu hiyo katika usajili mpya wa 2024/25.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema mchezaji huyo hayupo kwenye mipango ya timu kwa msimu mpya wa mashindano.

Amesema wamemalizana na mchezaji huyo kwa kumpa stahiki zake zote baada ya kuvunja mkataba wa miezi sita uliosalia na kumtakia kheri anapokwenda kwenye changamoto zingine.

“Jobe hayupo kwenye mipango yetu na tumeachana rasmi baada ya makubaliano ya pande zote mbili, tumemalizana na kila mmoja hakuna anayemdai mwezake, hii ni sehemu ya maboresho ya timu yetu,” amesema Ahmed.

Kikosi cha Simba kipo jijini Ismailia, Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ikiwa na washambuliaji, Kibu Denis, Freddy Michael, Steven Mukwala na Joshua Mutale ambaye anauwezo wa kucheza nafasi hiyo na kiungo mshambuliaji.

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button