Habari Mpya

KMC: Simba wakifika dau tunawaachia Awesu

DAR ES SALAAM: UONGOZI wa KMC FC umesema hawawezi kumuwekea ugumu kiungo wao Awesu Awesu na klabu ya Simba kwa kulipa kiasi cha fedha ambazo wanazihitaji kumuuza nyota huyo.

Awesu Awesu aliingia katika sintofahamu na timu yake hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kutumikia Simba SC kisha kuwekewa pingamizi na KMC.

Baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujiridhisha na kuamua nyota huyo  bado ni mchezaji halali wa KMC FC, na kama Simba SC inamuhitaji mchezaji huyo izungumze na klabu yake.

Ofisa Habari wa KMC FC, Khalid Chukuchuku, ameiambia Spotileo kuwa baada ya kupokea barua kutoka Kamati hiyo wakafungua milango kwa klabu inayohitaji huduma ya mchezaji huyo kwa ajili ya mazungumzo na mambo kuweka sawa.

Amesema suala la nyota huyo linaenda vizuri na kuwepo kwa mazungumzo kwa pande zote tatu huku Simba na Awesu kulipa kiasi cha fedha ili kuvunja mkataba.

“Awesu ni kijana wetu amefanya makubwa sana hapa KMC FC, hatuwezi kumkomoa, mazungumzo yanaendelea kwa pande zote mbili, kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo usiku kila kitu kitawekwa wazi,” amesema Khalid.

Inaeelezwa kuwa awali KMC FC ilihitaji kiasi cha million 200 ikiwa thamani ya mchezaji huyo ambapo mazungumzo yanaendelea kufanyika na kusalia katika Mill 170 kwa ajili ya kutoa barua ya kuachana na kuwa huru kuitumikia Simba

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button