Núñez afuta picha Instagram zinazohusiana na Liverpool
FOWADI wa Uruguay, Darwin Núñez, 24, amechochea uvumi wa kuondoka Liverpool majira haya ya kiangazi kwa kufuta picha zake zoke kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Instagram wakati akikiwasha Anfield. (90min)
Núñez alihamia Anfield kwa ada ya pauni milioni 85 majira ya kiangazi 2022. Amefunga mabao 33 katika michezo 94.(Goal.com)
Fowadi wa England, Jadon Sancho, 24, hataki kurejea Manchester United mwisho wa kipindi chake cha mkopo Borussia Dortmund. (Talksport)
Inter Milan inakusudia kusikiliza ofa za kumsajili beki wa kidachi Denzel Dumfries, 28, ambaye ana nia kujiunga na Manchester United. (La Gazzetta dello Sport – in Italian)
Chelsea imeimarisha nia kumsajili kiungo wa Ukraine anayecheza Shakhtar Donetsk Georgiy Sudakov, 21 anayekadiriwa kuwa na thamani na pauni mil 65 ambaye pia anafuatiliwa na Arsenal, Manchester City and Liverpool. (Mail)
Chelsea pia inataka kumsajili fowadi wa Nigeria anayekipiga Napoli, Victor Osimhen, 25, ambaye ana kipengele cha kuachiwa cha zaidi ya pauni mil 100. (Sky Italia – in Italian)