Ligi Kuu

Ahmed Ally: Simba tupo tayari kwa Pamba Jiji

DAR ES SALAAM: MENEJA Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kikosi cha timu hiyo kimekamilika kuelekea mchezo wa Jumapili dhidi ya Pamba Jiji baada ya nyota wote kurejea na kuwa katika hali nzuri.

Akizungumza kupitia mtandao wa Simba Ahmed amesema kurejea kwa wachezaji wote kunatoa faraja kwa benchi la ufundi na kuongeza ushindani ndani ya kikosi wakati timu ikijiandaa kwa mchezo huo muhimu.

“Nyota wote wamesharejea kamili na wote wako katika hali nzuri. Tunakwenda mechi ya Jumapili dhidi ya Pamba Jiji tukiwa tumekamilika,” amesema Ahmed.
Amesema kuwa hali ya wachezaji ni nzuri na maandalizi yanaendelea kama yalivyopangwa huku kila mmoja akiwa na ari ya kupambania matokeo chanya.

Simba inaendelea na maandalizi ya mwisho ya mchezo huo kwenye Uwanja wa KMC ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri dhidi ya Pamba Jiji na kuwa na mwendelezo mzuri wa kusaka matokeo mazuri ili kuendelea kujiweka pazuri katika mbio za ubingwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button