Nyumbani

Serikali yalenga Kudhibiti kamari Mpya wa Asilimia 5

DODOMA:WAZIRI wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, amesema Serikali inapendekeza kuanzishwa kwa ushuru wa bidhaa wa asilimia 5 kwenye thamani ya dau la kamari  zinazochezwa kupitia michezo ya kubashiri ya ardhini na mtandaoni, kasino za ardhini na mtandaoni, mashine za sloti pamoja na michezo ya vikaragosi (virtual games).

Akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri Khamisi amesema hatua hiyo inalenga kupunguza athari zinazotokana na michezo ya kubahatisha, ikiwemo uraibu wa kamari na kupungua kwa ushiriki wa vijana katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi.

Ameeleza kuwa asilimia 10 ya mapato yatakayokusanywa kutokana na ushuru huo yataelekezwa kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) ili kuimarisha usimamizi na udhibiti wa sekta ya michezo ya kubahatisha nchini.

Kwa mujibu wa Waziri Khamis, pendekezo hilo litasaidia kudhibiti athari za kijamii zinazohusishwa na kamari sambamba na kuongeza mapato ya Serikali kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo.

Serikali inatarajia kukusanya takribani shilingi bilioni 74.50 kutokana na utekelezaji wa ushuru huo mpya endapo mapendekezo hayo yataidhinishwa.

Related Articles

Back to top button