Liverpool yamwinda Rodrygo
TETESI za usajili zinaonesha Liverpool inataka kumsajili winga wa Real Madrid, Rodrygo Silva de Goes, maarufu Rodrygo na klabu hiyo ya Hispania itapokea ofa huku ikijiandaa na kuwasili kwa Kylian Mbappe kutoka Paris Saint-Germain majira yajayo ya kiangazi.(Fichajes)
Borussia Dortmund haina nia kumsajili tena Jadon Sancho iwapo winga huyo atachagua kuondoka Manchester United.(Bild)
Mchezaji anayeweza kuondoka Man Utd hivi karibuni ni kiungo Scott McTominay huku klabu hiyo ikikusudia kuachana na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Scotland kwa gharama yoyote. (Fichajes)
Hakuna kipengele cha kuachiwa katika mkataba mpya wa Joao Palhinha katika klabu ya Fulham, hali inayoleta utata wa uwezekano wa uhamisho kwenda Bayern Munich Januari, 2024.(Football Insider)
Manchester City na Real Madrid zote bado zina nia kumsajili Gabri Veiga. Kiungo huyo wa Hispania alishtua kwa uhamisho kwenda Al Ahli ya Saudi Arabia majira haya ya kiangazi lakini anaweza kupewa ofa ya kurejea Ulaya msimu ujao. (Fichajes)
Arsenal, Chelsea na Real Madrid zote bado zina nia kumsajili mshambuliaji wa Juventus, Dusan Vlahovic ambaye anaweza kuuzwa mwaka ujao. Ofa kutoka Chelsea inaweza kuongezeka wakati wa dirisha la uhamisho Januari, 2024.(Il Bianconero)
Barcelona inapanga kumsajili kiungo wa RB Leipzig Dani Olmo mwaka 2024. Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania anaweza kupatikana kwa ada ya Euro milioni 60 sawa na shilingi bilioni 157.7.(Fichajes)
Xavi Simons amekataa nafasi kurejea Manchester United majira haya ya kiangazi akipendelea kurejea Paris Saint-Germain. (Fabrizio Romano)