Tetesi

Tetesi za usajili

TIMU ya Arsenal inaanza kuchoshwa na Kai Havertz iliyomsajili majira ya kiangazi kutokana na kutoonesha kiwango bora tangu awasili Emirates wakati mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Jorginho anakaribia kuondoka klabu hiyo kipindi cha dirisha la uhamisho Januari, 2024.(Fichajes)

Uhusuano kati ya Jadon Sancho na kocha Erik ten Hag katika klabu ya Manchester United sasa haurekebishwi (i)

Chelsea inataka kusajili beki wa kushoto mwaka 2024 na imewaongeza kwenye orodha yake ya usajili Federico Dimarco wa Inter na Theo Hernandez wa AC Milan.(Calciomercato.it)

Beki kinda wa Lecce Patrick Dorgu ameivutia Chelsea ambayo itashindana na Liverpool kipindi kifupi kijacho kwa ajili ya saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18.(Fichajes)

Klabu za Saudi Arabia zinatarajiwa kuongoza kumfuatilia mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen Januari, 2024 mbele ya Chelsea na Real Madrid.(Mail)

Mshambuliaji mwingine katika rada ya Real Madrid ni nyota wa Tottenham Hotspur, Son Heung-min ambaye anafuatiliwa kwa karibu baada ya kuonesha kiwango bora msimu huu. (Fichajes)

Real Madrid inajiandaa kuingia vitani na Barcelona majira yajayo ya kiangazi kupata saini ya winga wa Athletic Club, Nico Williams. (Sport)

Manchester City inataka kumsajili kiungo wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz lakini kwa sasa mchezaji huyo mwenye umri wa 20 haonekani kutaka kuondoka Ujerumani. (SportBILD)

Baada ya ofa zake mbili kukataliwa, Paris Saint-Germain inajiandaa ofa ya tatu kumsajili Bernardo Silva wa Man City 2024 na haitaki kuacha ndoto ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno.(Le10Sport)

Kocha wa Roma, Jose Mourinho ana nia kuungana tena na beki wa Tottenham, Eric Dier Januari, 2024.(Calciomercato)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button