Amunike atamani Osimhen acheze PSG

NIGERIA, Lagos: WINGA wa zamani wa Super Eagles, Emmanuel Amunike, ameidhinisha uhamisho wa Victor Osimhen kwenda Paris Saint-Germain.
Mabingwa wa Ligue 1, PSG kwa sasa wanafanya kazi ya kumsajili Osimhen msimu huu wa joto.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 130 katika kandarasi yake.
Amunike, ambaye alimpa Osimhen mafanikio kimataifa alipokuwa katika timu ya taifa ya chini ya umri wa miaka 17, amesema kuhamia PSG kutasaidia maisha ya mshambuliaji huyo.
“PSG ni timu kubwa inayocheza Ligi ya Mabingwa ya UEFA, itakuwa jambo la kufurahisha na jema akihamia huko,” Amuneke alisema.
“Osmen amekuwa nijambo la kufurahisha baada ya kufanya mengi akiwa na Napoli. “Yeye ni nyota wetu hasa timu ya taifa Nigeria, lazima awe anacheza na pia awe ananajua anachotaka.”