Tetesi

Ayoub aipasua kicha Simba

DAR ES SALAAM. KIPA namba moja wa Simba, Ayoub Lakred anaendelea kuumiza vichwa vya mabosi wa timu hiyo kuhakikisha wanafanikiwa kumbakiza ndani ya kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi.

Kipa huyo ameonyesha uwezo mkubwa kwa msimu huu na kuitumikia klabu hiyo mwaka mmoja ambao umefikia tamati na sasa yupo huru na uongozi wa Simba kuhitaji kumuongeza mkataba mwingine.

Imeeleza kuwa viongozi wanapambana kuhakikisha wanambakiza kipa huyo kuendelea kusalia ndani ya Simba kwa msimu ujao licha ya kuanza mchakato mwingine wa kutafuata kipa mwingine wa ziada.

“Ayoub anatarajia kuondoka nchini na kwenda kwao kwa ajili ya mapumziko huku mazungumzo yakiendelea, wanapambana kuona kipa huyo anasailia tena Simba, lakini pia wanaangalia upande mwingine wa kuzungumza na baadhi ya makipa,” amesema mtoa habari huyo.

Amesema mipango yao baada ya Ayoub ni makipa wawili Luic Owono nchini Gabon na Ley {Matampi} kutoka Coastal Union ambaye msimu huu amekuwa kipa bora kwa kumzidi nyanda wa Yanga Djigui Diarra.

Spotileo lilimtafuta Ofisa Habari wa Coastal Union, Abbas Elsabri amesema Matampi, bado ana mkataba lakini wamesikia kuwa Simba wana nia ya kuhitaji huduma ya kipa huyo.

“Hatujapata ofa kutoka Simba, lakini nia yao ipo, endapo watakuja hatuna shida na tutakaa mezani na kumaliza dili kama ilivyo kwa beki wetu Lameck Lawi kumuuza kwa wekundu hao wa Msimbazi,” amesema Abbas.

Related Articles

Back to top button