Habari Mpya
Nimejipanga kuipigania Yanga-Morrison

MSHAMBULIAJI wa Yanga Bernard Morrison amewataka mashabiki wa timu hiyo kukaa kwa kutulia kwani kuna mengi amedhamiria kuifanyia timu hiyo msimu huu.
Akizungumza na Spotileo mchezaji huyo amesema malengo yake ni kushirikiana na wenzake kuifikisha timu hiyo mbali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Wapo watu wanahofu na mimi kwamba nitafanya vituko niwaambie tu hakuna kitu cha tofauti kitakachotokea nimejipanga kuipigania timu hii kufikia malengo yake katika mashindano yote,”amesema Morrison.
Amesema kwa ubora wa kikosi cha Yanga anaamini malengo yatafanikiwa.
Yanga ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara, ngao ya jamii na itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.