Habari Mpya

Muigizaji Hawa maarufu Carina afariki dunia India

INDIA: MUIGIZAJI wa filamu nchini, Hawa Hussein Ibrahim maarufu Carina, amefariki dunia leo Aprili 15,2025 akiwa nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu ya tumbo.
Carina alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya tumbo kwa zaidi ya miaka tisa na kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara 24.Aliondoka nchini Februari 24, 2025 kwenda India kupatiwa matibabu baada ya kukamilika kwa taratibu za safari na gharama ya matibabu ya Sh milioni 54 ambazo zilitokana na msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, michango ya taasisi mbalimbal na watu mbalimbali.

Kabla ya kuondoka, Carina alitoa shukrani kwa wote waliomsaidia. Hata hivyo, Carina alitarajiwa kurejea nchini leo baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa kutibu tatizo la tumbo lililokuwa likimsumbua kwa kipindi cha miaka tisa, huku akifanyiwa upasuaji wa tumbo mara 24.

Matumaini ya kupona na kurejea salama yamekatizwa na taarifa ya kifo chake. Pumzika kwa amani Hawa Hussein Ibrahim maarufu Carina.

Related Articles

Back to top button