Habari Mpya

Rashid amwaga wino Pamba

KATIKA juhudi za kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya klabu ya Pamba ya Mwanza inayoshiriki ligi ya Championship imemsajili Mohamed Rashid.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Pamba imesema inaendelea kufanya usajili bora kwenye kikosi chake kwa kuchanganya wachezaji wachanga na wenye uzoefu wa kutosha.

“Tunayofuraha kuwatambulisha kwemu nyota wetu mpya Mohammed Rashid ambaye anajiunga nasi kuhakikisha tunafanikiwa kucheza NBCPL msimu Ujao,”imesema Pamba.

Kwa mujibu wa Pamba Mohammed Rashid ametumikia kwa nyakati tofauti Tanzania Prisons, Simba na JKT Tanzania.

Dirisha la usajili kwa klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligu Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite(SWPL) msimu wa 2022/2023 linatarajiwa kufungwa Jumatano Agosti 31, 2022 saa 5.59 usiku.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button