Nyumbani

Ngoma, Mzamiru wajipange

KUNA kazi kubwa kwenye safu ya viungo wakabaji wa Simba, hasa kwa nyota Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma kutokana na usajili mpya wa kiungo, Debora Fernandes ndani ya klabu hiyo.

Simba imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji huyo kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea klabu ya Mutondo Stars ya Zambia.

Usajili wa Debora unaenda kuwapa wakati mgumu viungo waliopo ndani ya kikosi hicho , Mzamiru, Ngoma na Sadio Kanoute.

Akizungumza na Spotileo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema Debora anamudu kucheza kiungo mkabaji (namba sita) ingawa anafurahi kucheza namba nane.

Amesema ujio wa kiungo huyo unaongeza nguvu katika eneo hilo, anauwezo wa kuzuia na kupiga pasi sahihi kuelekea mbele na kuanzisha mashambulizi.

“Tunaendelea kusuka timu imara kwa ajili ya muda mrefu maana ya usajili wetu umezingatia umri wa wachezaji wanaosajiliwa, kwa kuongeza mtu katika kila idara na kuifanya Simba bora,” amesema Ahmed.

 

Related Articles

Back to top button