Nyumbani

Yanga, Coastal Union: Vita ya kufuzu 16 bora Kombe la Shirikisho

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Yanga SC kinashuka dimbani leo katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, kupambana na Coastal Union kwenye hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB (FA).

Mchezo huo ni muhimu kwa pande zote mbili, kwani mshindi atafuzu kucheza hatua ya 16 bora, kuungana na timu zilizotangulia kama Mbeya City, Stand United, Singida Black Stars, Tabora United, Mashujaa FC, Mbeya Kwanza, na Mtibwa Sugar.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hamdi Miloud, amesema kuwa wamejiandaa kwa umakini mkubwa kuelekea mchezo huo, wakijua kuwa Coastal Union ni timu yenye ubora na wachezaji wenye uzoefu.

“Tumefanya maandalizi mazuri. Tunajua hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu Coastal Union ni timu yenye wachezaji bora. Hata hivyo, tunahitaji ushindi ili kufikia malengo yetu,” amesema Miloud.

Kwa upande wa Coastal Union, Kocha Juma Mwambusi amesema kikosi chake kiko njiani kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo.

Amethibitisha kuwa wanajua ugumu wa mchezo dhidi ya Yanga lakini wako tayari kupambana na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua, huku kila timu ikihitaji ushindi ili kusonga mbele katika michuano hii ya FA Cup.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button